Signal ni programu ya utumaji jumbe yenye msingi wa faragha. Hailipishwi na ni rahisi kutumia, huku ikiwa na usimbaji fiche thabiti unaofanya mawasiliano yako kuwa ya faragha kabisa.
• Tuma jumbe, jumbe za sauti, picha, video, vibandiko, GIFs, na mafaili bure. Signal hutumia muunganisho wa data wa simu yako, ili uepuke tozo za SMS na MMS.
• Wapigie marafiki wako kwa kutumia simu za sauti zilizosimbwa na simu za video. Simu za vikundi zinazopokea hadi watu 50.
• Kaa katika muunganiko wa magumzo ya makundi ya hadi watu 1,000. Thibiti nani anayechapisha na kusimamia wanachama wa kikundi kwa mipangilio ya ridhaa ya admin.
• Share stori za picha, jumbe na video zinazotoweka baada ya saa 24. Mipangilio ya faragha hukupa udhibiti wa ni nani hasa anayeweza kuona kila Stori.
•Signal imetengenezwa kwa ajili ya faragha yako. Hatujui chochote kuhusu wewe au unayezungumza naye. Protokali yetu ya wazi ya Signal inamaanisha kuwa hatuwezi kusoma jumbe zako au kusikiliza simu zako. Vile vile hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza. Hakuna milango ya nyuma, ukusanyaji data wala majadiliano.
•Signal inajitegemea na si ya kibiashara; ni kampuni ya kiteknolojia tofauti inayotoka shirika la kitofauti. Kama shirika lisilo la faida la 501c3 tunaungwa mkono na michango yako, si watangazaji biashara au wawekezaji.
• Kwa msaada, maswali na taarifa zaidi tafadhali tembelea https://support.signal.org/
Ili kuangalia kodi yetu ya chanzo, tembelea https://github.com/signalapp
Tufuate Twitter @signalapp na Instagram @signal_app
Ilisasishwa tarehe
22 Apr 2025
Mawasiliano
Usalama wa data
arrow_forward
Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Hakuna data inayoshirikiwa na wengine
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha kushiriki data
Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
Taarifa binafsi
Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
Unaweza kuomba data hiyo ifutwe
Angalia maelezo
Ukadiriaji na maoni
phone_androidSimu
laptopChromebook
tablet_androidKompyuta kibao
4.5
Maoni 2.65M
5
4
3
2
1
Makeresia Pawa
Ripoti kuwa hayafai
Onyesha historia ya maoni
3 Septemba 2021
Nzuri
Watu 6 walinufaika kutokana na maoni haya
Vipengele vipya
★ Tumeweka njia ya mkato rahisi ili uweze kushusha mkono haraka ukianza kuongea kwenye simu ya kikundi kwa Signal. Ni kipengele kinachopendwa zaidi katika toleo hili.