Mfuko Rangi ni kihariri rangi ambacho, kati ya vingine, huruhusu kurekebisha sehemu za picha ili kua angafu na kuikuza hadi kiwango cha pikseli.Imeunganishwa na Msimbo wa Mfukoni---
https://play.google.com/store/apps/details?id=org.catrobat.catroid --- lakini inaweza pia kutumika yenyewe.
Picha zinahifadhiwa kwenye nyumba ya sanaa na pia kwenye kabrasha ya\"Mfuko Rangi\"
Mfuko Rangi umeundwa na mradi wa Catrobat ambao ni huru na wazi usio wa kibiashara --- http://catrobat.org/
Furahia!
Vipengele:
-Muundo wa picha:png yenye uangafu.
-Vifaa:brashi, pipette, muhuri, duara/duara dufu, kukata, kugeuza, kukuza, kifaa mstari, mshale, kifaa jaza, mstatili, kuingiza picha, kifutio, kuhamisha, na kuzungusha.
-Kuchora kwenye skrini nzima.
-Upana na umbo la mstari.
-Kibao cha rangi au thamani ya RGBa
Unataka kutusaidia kutafsiri Mfuko Rangi kwenye lugha yako?.Tafadhali wasiliana nasi kupitia translate@catrobat.org tueleze ni lugha gani unaweza kutusaidia.Hata lugha zisizohamasishwa kwenye Android moja kwa moja zinakaribisha. Tuanafanya kazi ili kubadilisha lugha hizi.
Sisi sote ni wafanyakazi wa kujitolea kwa kutumia muda wetu bila malipo yoyote kwenye mradi huu huria na wazi kwa lengo la kuongeza ujuzi wa fikra za kimahesabu kati ya vijana na watoto duniani kote.Programu yetu itabaki kuwa bila matangazo na bila gharama ,hivyo tafadhali tunaomba mtuwie radhi tukishindwa kurekebisha makosa au kuongeza vipengele haraka.Kwa upande mwingine hili linawezesha mradi kubaki huru na ufadhili wowote na inahakikisha kwamba unaweza kuendelea milele , ¬hivyo hakuna hatari ya kuwa tutazuiliwa kuendeleza mradi huu.Tayari wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 300 wamechangia mpaka sasa kwenye mradi wetu.
Itatuasaidia sana kama utatoa vizuri kiwango na tathimini yetu kwenye Google Play,viwango na tathimini hizi zitasaidia watumiaji wapya kutumia programu yetu.Kwa bahati mbaya, viwango vilivyotolewa awali havikua vizuri kutokana na makosa ambayo tayari yametatuliwa au vipengele vilivyosahaulika awali ambavyo haviwezi kuondoka,hivyo ni vigumu sana kuondoa viwango vibaya hata kama hayo makosa yamesharekebishwa muda mrefu.Hivyo tafadhali , tusaidie kwa kutoa viwango na tathimini nzuri:-)
Ilisasishwa tarehe
2 Jul 2024